Skip to main content

JINSI YA KUSAJILI KAMPUNI

JINSI YA KUSAJILI KAMPUNI

UTANGULIZI
Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi.

Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia.

HATUA 10 ZA USAJILI
Hatua #1: Taarifa za msajili

Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa).

Taarifa zenyewe ni:-

  1. Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni
  2. Simu ya kiganjani
  3. Barua pepe yaani email
Hatua #2: Taarifa za kampuni
Taarifa za kampuni zinazotakiwa ni:-

  1. Aina ya kampuni kama ni ya hisa au isiyo na hisa, ya binafsi au ya uma nk
  2. Jina la kampuni
  3. Tarehe ya kufunga mahesabu - mfano 31 Desemba
  4. Kumbuka: TIN No., Namba ya usajili zitawekwa na mfumo automatically
Hatua #3: Ofisi za kampuni
Taarifa za ilipo au itakapokuwa ofisi za kampuni ambazo ni:-

  1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
  2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
  3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
  4. Sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #4: Shughuli za Kampuni
  • Taja shughuli za kampuni kama ilivyoorodheshwa kwenye mfumo wa ISIC Classification
Hatua #5: Taarifa za wakurugenzi
Taarifa zinazotakiwa za Wakurugenzi ni:-

  1. Aina ya mkurugenzi kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. TIN
  5. Simu ya kiganjani
  6. Barua pepe yaani email
  7. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuanii ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namaba ya kiwanja, kitalu na nyumba,
  8. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
Hatua #6: Taarifa za katibu wa kampuni
Taarifa za katibu wa kampuni (company secretary) zinazotakiwa ni:-

  1. Aina ya mtu kama ni mtu asili au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya kiwanja, kitalu na nyumba, sanduku la posta, simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email
  7. Simu ya ofisi/kiganjani na barua pepe -email na (sanduku la posta kwa ajili ya memart)
Hatua #7: Taarifa za wanachama/wenye hisa
Taarifa za wanachama au wenye hisa zinazotakiwa ni:-

  1. Aina ya mtu kama ni mtu au taasisi
  2. Asili yake kama ni mwenyeji au mgeni
  3. Kitambulisho cha taifa kama ni mwenyeji au passport kama ni mgeni
  4. Simu
  5. Barua pepe - email
  6. Anuani ya makazi kwa kila mkurugenzi kwa kufuata mfumo wa anuani ya ofisi hapo juu
    1. Taarifa za za makazi zinazotakiwa ni:-
      1. Aina ya eneo (Aidha limepimwa au la)
      2. Kama halijapimwa tayarisha anuani ya makazi yenye mfumo huu, jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji, kitongoji na ueleze kama eneo lipo karibu na alama zipi ambazo hazihamishiki kama shule ya msingi nk. Usiweke alama ambazo hazina uhakika wa kudumu hapo maana brela watazikataa)
      3. Kama limepimwa tayarisha yafuatayo: Jina la Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji/mtaa, barabara, namba ya
Hatua #8: Viambatanisho (Attachments in PDF)
Viambatanisho vinavyotakiwa kuambatanisha kwenye maombi (zote katika pdf) ni:-

  1. Memorandum and articles of association iliyosainiwa na wanachama/wenye hisa pamoja na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  2. Form 14b iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi na mwanasheria wa uma (Notary Public)
  3. Ethics and Integrity Forms iliyosainiwa na mmoja wa wakurugenzi
  4. Company consolidated form iliyosainiwa wakurugenzi wote na katibu wa kampuni
Hatua #9: Ada za usajili na kufaili (Different Fees)
Aina za ada ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini

  1. Kusajili kampuni
  2. Kuhifadhi nyaraka na
  3. Stamp Duty
Hatua #10: Namna ya kulipa ada (Payment Methods)
Malipo ya ada yanafanyika kwa njia kuu tatu ambazo ni

  1. Kuweka Benki: Kwa njia y kuweka Fedha kwenye Tawi la Benki /Wakala wa Benki
    Nenda kwenye Tawi lolote la Benki / Wakala wa Benki ya CRDB /NMB kwa kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  2. Kwa njia ya Simu ya Mkononi: Tumia mtandao wa simu wa AirTell Money / Tigopesa/ MPesa/ HalloPesa kwa kuweka namba ya Kampuni 888999 na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
  3. Kwa njia ya Kuhamisha Fedha: Unaweza kuhamisha Fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti zetu zilizoko katika Benki ya NMB/ CRDB kwa njia ya TISS /SWIFT kwa kujaza: Namba ya Akaunti na Kumbukumbu ya Malipo uliyopewa kupitia PO yako
Kumbuka: Utaratibu wa malipo aidha kwa simu au benki utapewa ukishafikia hatua husika ya malipo


HITIMISHO NA USHAURI
Brela sasa hivi hawataki usajili kwa njia ya zamani, yaani kupeleka makaratasi ngumu na kusubiri mlangoni kwa siku 6. Pia BRELA hawakubali mtu asiye na kitambulisho cha Taifa yaani #NIDA kusajili kampuni au jina la biashara.
Taarifa zilizotolewa hapo juu ni zile za lazima ambazo bila hizo huwezi kumalizia usajili na au usajili unaweza kukawia

Nashauri yafuatayo:

  1. Nashauri kama unataka kusajiliwa kampuni au jina la biashara kwa haraka wasiliana nasi kwa kutumia 
  2. Kama huna kitambulisho cha Taifa na umeshaandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, tembelea ofisi zozote za NIDA karibu na wewe ili wakupe angalau namba yako ya kitambulisho ili uweze kukitumia ukiambatanisha na Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  3. Nashauri pia kama bado hujajiandikisha ni vyema ukawahi, hata kupitia kwenye eneo ambalo zoezi linaendelea ili uwahi kwa maana serikali imeanza kuzuia kupata huduma za public kama huna kitambulisho. ambatanisha pia Kibali cha BRELA ili Kupata Kitambulisho cha NIDA kwa haraka.
  4. Mwisho nashauri hizi taarifa zote uwe nazo mkononi kwa sababu huu mfumo wa usajili wa ORS unakupa siku sita (6 days) tu kukamilisha usajili kama baada ya hizo siku bado, taarifa zote zinafutika na itakubidi uanze upya from the scratch.

Comments

Popular posts from this blog

Nafasi 68 za Kazi Rinsen Consultancy

New Jobs at Rinsen Consultancy | Ajira mpya 2020 1. Position:  Cabin Crews ( 32 positions ) Organization:  Rinsten Consultancy Co. LTD Reports to : Head Of Operations Scope of Work As a Cabin Crew with our Client, you will be part of an airline that has won more than 100international awards for excellence, awards that say that they are the best. You will be based in either one of the following Cities; DAR ES SALAAM, DODOMA, MOMBASA, NAIROBI, MWANZA, KISUMU, ELDORET, MBEYA, ENTEBE, KAMPALA, KILIMANJARO( KIA ), MTWARA & BUKOBA. Reccomended: P ATA LOGO YA BIASHARA YAKO BURE HAPA Our Client operates one of the latest wide-bodied Boeing and Airbus aircrafts to a constantly growing network of key cities on every continent. You will enjoy high standard apartments, full medical care and state-of-the-art facilities in training and at work. Our Client gives a lot but asks a lot, too. Cabin Crews need to be dynamic and passionate about being the best; innovative and tireless in s...

Nafasi 7 za Kazi Agricultural Markets development Trust (AMDT)

Ajira Mpya 2020 | New Jobs 2020 Overview The Agriculture Markets Development Trust ( AMDT ) has been established by the Governments of Denmark, Ireland, Sweden and Switzerland in 2014 and the current Trustee is KPMG. The Trust has been established as a long term facility with the overall objective of increasing incomes and employment opportunities for poor women, men, and young people in Tanzania. With a strong pro-poor focus, the Trust works with the Private Sector, Government and Civil Society Organisations to promote the making Markets Work for the Poor (M4P)/Market Systems Development (MSD) approach that stimulates changes to market systems leading to broad and sustained impact on the lives of smallholder farmers as well as competitiveness of agricultural MSMEs. AMDT achieves this by investing, together with market actors, in interventions that are: (i) based on diagnosed constraints and pro-poor opportunities, (ii) are well coordinated to enhance the leveraging of investments and ...

Nafasi 4 za Kazi Lake Victoria Fisheries Organization (LVFO)

  Background Lake Victoria Fisheries Organization (LVFO) is an institution of the East African Community (EAC) charged with the management and development of fisheries and aquaculture. It was formed by a Convention in 1994 with major amendments in 2016. It is accommodated under Article 9.3 of EAC Treaty and registered as a Regional Fisheries Management Organization (RFMO) under the FAO UN Charter CAP 102. The overall objective of the LVFO is to promote sustainable management and development of the fisheries and aquaculture in order to contribute to food security and economic growth in the EAC region. The 2016 amendment to the Convention that established LVFO expanded her mandate and scope to cover among others issues of fish quality, trade, and marketing. In addition, as EAC Partner States submit their instruments of accession to the Repository (FAO) and join the Organization, the number of main stream and project staff increases. Against this background, LVFO Secretariat is seekin...