USAJILI WA BIASHARA
Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Utoaji Leseni BRELA ilianzisha mfumo mpya wa usajili wa Biashara (Jina la Biashara na Kampuni) unaoitwa ORS yaani Online Registration Sytem. Huu ni mfumo unaokuwezesha kusajili Jina la Biasahara au Kampuni kwa njia ya mtandao ukiwa popote katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tofauti kati ya JINA LA BIASHARA na KAMPUNI
Jina la biashara ni jina unaloipa biashara yako kwa ajili ya kuitambulisha biashara kwa wateja wako. Jina la biashara ni sehemu muhimu ambayo inagusa hisia za mteja deep down, jaribu kufikiria ukisikia jiana "Apple" ni nini kinakuja kwenye kichwa na moyo wako? Vipi kuhusu "Dangote"? au "Gucci"?. Utagundua majina haya ya biashara huwa mara nyingi ni mafupi yameambatana na Logo na chini yake kauli mbiu ya biashara.
Unawezaje kuchagua jina sahihi la Biashara yako? Kitu cha kwanza ni kuchagua jina ambalo linawakilisha au lina uhusiano mkubwa na huduma au biashara unayofanya mfano jina "Lunchtime Hotel", "Vodacom", "Rungu", "Temptation" n.k. Kitu cha pili ni kuzingatia urefu wa jina lako, ni vizuri ukachagua jina ambalo ni fupi ili lisiwape shida wateja na iwe rahisi kwa watoto na wakubwa kulisoma lakini pia wanaojua kusoma na wasiojua kusoma mfano "TECNO". kitu cha tatu angalia upekee wa jina, usichague jina litakalokuingiza kwenye migogoro na majina mengine ya biashara. Majina ya biashara yanalindwa na sheria kwa maana ya kwamba kama utatumia jina la mtu mwingine utaingia kwenye ugomvi. Kitu cha nne zingatia mahitaji ya baadae je biashara yako itakuwa kubwa kiasi gani baadae? kama una mpango wa kutanua wigo wa biashara yako baadae usichague jina lenye kulimit bidhaa moja.
Gharama za Usajili wa Jina la Biashara
Nahusika na kuwasaidia watu kusajili majina ya kampuni au biashara BRELA kupitia website ya ors.brela.go.tz.
Gharama za usajili zinahusisha maeneo yafuatayo:
- Gharama za BRELA = 20,000/=.
- Gharama za mtaalam 30,000/=
- Jumla ya Gharama ni 50,000/=
Faida za Kusajili Jina la Biashara
1. Kurasimisha biashara yako Kwa mujibu wa Sheria (Biashara yako inakuwa rasmi)
2. Unaweza kufungua Akaunti ya biashara BANK na kuipa jina la biashara na kujifungulia milango ya kupata MIKOPO kwa ajili ya kukuza biashara yako.
3.Jina hili litalindwa na hakuna mtu mwingine yoyote atakayeweza kulitumia.
Nifuatilie kwenye Makala Ijayo katika Mwendelezo wa mada hii
Contacts:
Phone: +255742751265
EMAIL: Ambitplus@gmail.com
Recommended
Nataka kufungua kampuni lakini nashindwa nianzie wapi
ReplyDeleteNipigie 0654502089
ReplyDelete