JINSI YA KUSAJILI KAMPUNI UTANGULIZI Kuanzia tarehe 1 Februari 2018 #BRELA ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wake wa kuwawezesha wamiliki wa makampuni kusajili na kuwasilisha returns BRELA. Pia BRELA ilishatangaza kwamba mnamo tarehe 25 Machi 2018 mfumo wake wa awali wa OBRS uliokuwa unaruhusu kusajili jina la biashara na kufanya clearance ya jina la kampuni kupitia website ungefungwa rasmi ili kuuruhusu mfumo mpya wa ORS wenye uwezo wa kusajili majina ya biashara na makampuni kufanya kazi rasmi. Hatua 10 za kufuata ili kusajili kampuni imeelezwa hapa chini, tafadhali fuatilia. HATUA 10 ZA USAJILI Hatua #1: Taarifa za msajili Ili kutumia mfumo huu mpya wa ORS mteja (msajili) anayetaka kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa na taarifa za msajili (msajili anaweza kuwa ni mmoja wa wakurugenzi, Katibu au Wanachama/Wenye hisa wa Kampuni tarajiwa). Taarifa zenyewe ni:- Kitambulisho cha Taifa kwa wenyeji na Passport kwa wageni Simu ya kiganjani Barua pepe ya...
AJIRA MPYA 2020 | NAFASI ZA KAZI | AJIRA ZETU | NEW JOBS